BY ISAYA BURUGU 11TH OCT 2023-Afisa mmoja wa polisi amefariki  kwa kujitoa uhai baada ya kujipiga risasi kichwani katika makao makuu ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) jijini Nairobi. Wenzake walisema alijifungia ndani ya gari lake na kujipiga risasi kichwani kwa bastola yake kwenye eneo la maegesho. Alikufa papo hapo.

Haijabainika mara moja sababu ya afisa huyo ambaye ni dereva wa polisi alichukua hatua hiyo kali. Wenzake waligutushwa na mlio wa risasi kutoka sehemu ya kuegesha magari kwenye sehemu ya shughuli na waliposongea walimkuta tayari amekufa.

Mwili wake ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi. Maafisa wakuu walikuwa ofisini wakati wa kisa hicho. Hili ni tukio la hivi punde zaidi kutokea katika huduma ya polisi. Wiki iliyopita, afisa mkuu alifariki kwa kujitoa uhai nyumbani kwake eneo la Utawala, Nairobi.

Superintendent Ezra Ouma alijipiga risasi nyumbani kwake alasiri ya Alhamisi Oktoba, 5 muda mfupi baada ya kumpigia simu rafiki yake ambaye pia ni afisa wa polisi na kumwambia angekufa kwa kujiua.

Share the love
October 11, 2023