Radio Osotua › Local News

Awamu ya pili ya uzinduzi wa miradi ya CIDP, Narok yaanza rasmi.

Miradi hii ya CIPD, ni sehemu ya miradi 64 ya maendeleo itakayozinduliwa baada ya zaidi ya miradi 363 kuzinduliwa katika awamu ya kwanza

Local News May 23, 2023 John Waicua

Serikali ya kaunti ya Narok imezindua miradi kadhaa ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya eneobunge la Narok Kaskazini, huku awamu ya pili ya miradi ya maendeleo ya kaunti CIDP iking’oa nanga rasmi hii leo.
Baadhi ya miradi iliyozinduliwa hii leo ni pamoja na ujenzi wa barabara, madarasa na vituo vya afya. Waziri wa barabara katika kaunti ya Narok John Gatua alizindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Kistoo-Olorupa na kusimamia uzinduzi wa zoezi la ukarabati wa Kituo cha Afya cha Enabelbel.
Miradi hii ni sehemu ya miradi 64 ya maendeleo inayotarajiwa kuzinduliwa katika awamu ya pili ya miradi hii ya maendeleo, baada ya zaidi ya miradi 363 kuzinduliwa kote katika kaunti ya Narok kwenye awamu ya kwanza.