Baraza la Magavana (CoG) limekosoa vikali mpango wa kukamatwa kwa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, likizua wasiwasi kuhusu kile walichosema ni kuongezeka kwa vitisho kutoka kwa kamati ya Seneti.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa baraza hilo Ahmed Abdullahi aliikosoa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) kuhusu mazingira yaliyozunguka kukamatwa kwa Sakaja na kushutumu baadhi ya maseneta kwa kukiuka mamlaka yao ya usimamizi.
Abdullahi alidai kwamba vitendo vya wanachama wanne wa kamati ya Seneti ni vitisho na majaribio ya kuwanyang’anya pesa magavana, akidai kwamba mwenendo huo umeathiri viongozi wengi wa kaunti.
Vilevile alipinga mwaliko wa magavana 29 na Kamati ya seneti ya Hesabu za Umma akielezea hatua hiyo kuwa isiyofaa na inayoendeshwa kisiasa.Baraza hilo lilidai kuondolewa mara moja kwa hati za kukamatwa zilizotolewa dhidi ya magavana.
The Council of Governors has called for the immediate withdrawal of the warrant of arrest against H.E Johnson Sakaja or coercive measures against Governors over non-appearance before the Senate’s County Public Accounts Committee (CPAC).
Addressing the press, @CogChair noted that… pic.twitter.com/tsyA8rC6xs— Council of Governors (@KenyaGovernors) March 31, 2026
HAPPENING NOW: Press briefing by the CoG Chairperson H.E FCPA Ahmed Abdullahi on Non-appearance of Governors before the Senate CPAC Committee https://t.co/Vde9Zh996l
— Council of Governors (@KenyaGovernors) March 31, 2026

