Radio Osotua › Local News

David Keter Aibuka Mshindi Emurua Dikirr.

Local News May 15, 2026 Brigit Agwenge

Mgombea wa UDA David Kipsang Keter ametangazwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa eneo la Emurua Dikirr uliofanyika Alhamisi.Tume ya IEBC ilisema kuwa Keter alipata kura 18,266 huku mpinzani wake wa karibu, Vincent Kibet Rotich wa Chama cha DCP, akipata kura 10,760.

Wagombea wengine katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Gideon Koech wa Chama cha NVPK, ambaye alipata kura 190, huku Desma Cherono wa PNU akipata kura 80. Kiprono Rotich wa chama cha RLP akifuata kwa kura 62.

Uchaguzi huo mdogo ulifanyika kufuatia kifo cha mbunge wa zamani wa Emurua Dikirr Johanna Ngeno, ambaye alipoteza maisha yake katika ajali ya ndege mwezi Februari mwaka huu.

Wakati huo huo, katika Kaunti ya Elgeyo/Marakwet, Festus Korir Kiprop wa Chama cha UDA alitangazwa mshindi wa CAW ya Wadi ya Endo baada ya kupata kura 4,475. Mpinzani wake wa karibu wa Chama cha Kidemokrasia cha Taifa (NDP) Shadrack Kosgei Chelang’a alipata kura 752.

Katika Kaunti ya Samburu, Daniel Lolngojine wa Chama cha UDA alishinda CAW ya Wadi ya Porro kwa kura 2,328, mbele ya Josphat Jumanne Leleur wa Chama cha KANU aliyepata kura 1,036.

Kati ya wapiga kura 6,358 waliojiandikisha, kura 4,194 zilipigwa na hivyo kuwafanya wapiga kura kujitokeza kwa 65.96%.