Radio Osotua › Narok County

Emurua Dikirr Yafanya Maamuzi.

Narok County May 14, 2026 Brigit Agwenge

Zoezi la upigaji kura liliandaliwa leo katika eneo la Emurua Dikkir ambapo wakaazi wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo ili kuchagua mbunge mpya.

Kiti cha ubunge cha Emurua Dikkir kilisalia wazi kufuatia kuaga dunia kwa aliyekuwa mbunge wa eneo hilo marehemu Johanna Ng’eno katika ajali ya ndege mapema mwaka huu.

Mwaniaji wa kiti cha ubunge eneo la Emurua Dikirr Transmara Mashariki David Keter maarufu Dolaline amewarai wakaazi wa eneo hilo kudumisha amani hata baada ya Uchaguzi.

Akizungumza baada ya kupiga kura katika kituo cha Chemelei, Bw.Keter pia amewataka maafisa polisi kuhakikisha kuwa usalama umeimarishwa hadi pale mshindi atakapotangazwa.

Kwa upande wake mwaniaji wa kiti hicho cha ubunge kwa tikiti ya DCP Vincent Rotich aliibua malalamishi kuhusu hatua ya baadhi ya maanjeti wake kuzuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura zoezi hilo lilipoanza.