BY ISAYA BURUGU 8TH SEPT 2023-Watu wanane wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa  usiku wa kuamkia leo baada ya matatu kugongana na lori eneo la Mlima Kiu huko Makueni kwenye Barabara Kuu ya Nairobi- Mombasa.

Akidhibitisha ajali hiyo ya saa tano usiku , Kamanda wa Polisi wa Makueni, Barbanas Ng’eno alisema abiria hao wanane walifariki papo hapo kufuatia ajali hiyo ya ana kwa ana.Matatu hiyo ilikuwa ikielekea Nairobi kutoka Loitoktok huku lori hilo likielekea Mombasa.

Miili ya marehemu hao ilihamishiwa katika Hospitali ya Kilungu huku mabaki ya magari hayo yakivutwa hadi Kituo cha Polisi cha Salama huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Hii sasa inafikisha 20 jumla ya idadi ya watu waliofariki kufuatia ajali za barabarani katika Barabara Kuu ya Nairobi Mombasa ndani ya saa 24 zilizopita.

Awali jana watu 12 waliuawa katika eneo la Ndii huko Taita Taveta  baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kugongana na lori.Dereva wa matatu aliripotiwa kujaribu kuyapita magari mengine   kabla ya kugongana na lori lililokuwa likija

 

Share the love
September 8, 2023