Jopo lililoundwa ili kuchunguza utendakazi na mienendo ya makamishna wanne wa tume ya IEBC,  imependekeza kuondolewa kwa kamishna aliyesalia wa tume hiyo Irene Masit baada ya kumpata na hatia ya madai kadhaa ya utovu wa nidhamu.

Jopo hilo ambalo lilikua likiongozwa na jaji Aggrey Muchelule, limeeleza kwamba halikuridhishwa na majibu aliyowasilisha mbele yake wakati akijitetea, na kuongeza kwamba alishindwa kudumisha uwazi, uwajibikaji kuishi kwa mujibu wa kiapo chake katika jukumu lake kama kamishna wa IEBC.

Jopo hilo aidha liliongeza kuwa, mienendo yake iliharibu mwonekano wa chama cha IEBC Mbele ya macho ya wananchi, na kupunguza imani yao kwa chama hicho. Masit alikuwa kamishena wa pekee aliyesalia katika tume ya IEBC kati ya makamishena wanne waliopaswa kuchunguzwa, na hii ni baada ya wenzake 3 kujiuzulu kabla ya kuanza kwa uchunguzi dhidi yao.

February 27, 2023