Radio Osotua › Local News

Kongamano la kitaifa la kilimo cha maembe laanza rasmi mjini Wote kaunti ya Makueni

Local News May 16, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,16TH MAY 2023-Kongamano la kitaiafa kujadili kilimo cha maembe limeanza rasmi hivi leo mjini Wote kaunti ya Makueni.Ni kongamano la siku tatu na limewavutia washikadau kutoka kaunti 15 ambapo maembe hukuzwa kwa wingi.

Mathumuni ya kongamano hilo ni kuzungumzia kilimo cha maembe ambapo washiriki watakuwa wanajadili jinsi ya kuboresha kilimo hicho,kusaka soko  na mbbinu bora za kutunza Maembe.

Waziri wa Kilimo kaunti ya Makueni Joyce Mutua anasema nia yao ni kurekebisha changamoto ambazo zimekuwa zikikumba kilimo cha maembe na haswa kuongeza dhamani bali na soko.