Zaidi ya wanafunzi laki moja walioandika mtihani wa KCSE mwaka uliopita walituma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu na taasisi za Anuwai kupitia tovuti ya KUCCPS.
Akitangaza matokeo ya uteuzi wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa mwaka 2026/2027, Waziri wa Elimu Julius Ogamba amesema kuwa jumla ya wanafunzi 293,869 wameteuliwa katika programu za shahada, stashahada na kozi za kiufundi.
Vilevile kati ya idadi hiyo, kuna wale ambao wameteuliwa kujiunga na taasisi ya mafunzo ya matabibu KMTC huku wengine wakitarajiwa kujiunga na taasisi za mafunzo ya walimu TTC.
This year, 980,535 students who sat Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) in 2025 were given an opportunity to apply for placement to any of their desired programmes and institutions. Of these, 268,729 attained mean grade of C+ and above and therefore qualified for…
— The Placement Service (@KUCCPS_Official) July 8, 2026
Aidha wanafunzi wengine 8,915 waliofuzu kwa program ya shahada, walituma maombi ya kujiunga na vyuo vya Anuwai. Kando nahayo, KUCCPS imesema kuwa kozi ya Shahada ya Tiba ilikuwa na ushindani mkubwa katika nafasi za 2026/2027.
Afisa Mkuu Mtendaji wa KUCCPS Agnes Wahome alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 6500 waliotuma maombi ya kosi ya udaktari, kulikuwa na nafasi kwa wanafunzi 702 pekee katika vyuo vikuu vyote vya umma na vya kibinafsi nchini Kenya, na kufanya mchakato huo kuwa wa ushindani mkubwa.
KUCCPS CEO Dr. Agnes Mercy Wahome: We have seen a steady increase in the number of students qualifying for university. We can account for 81% of the students who attained C+ and above in the 2025 KCSE examination. #KUCCPS #2026UniversityPlacement pic.twitter.com/Tc24NTYMlI
— The Placement Service (@KUCCPS_Official) July 8, 2026

