BY ISAYA BURUGU,11TH MARCH,2023-Lori lililokuwa limepakiwa  kwenye barabara ya  Kakamega-Kisumu  karibu na makao makuu ya serikali ya kaunti ya  Kakamega   imebingiria na kuangukia magari mawili yaliyokuwa    yamepakiwa  karibu na makao makuu ya kaunti hiyo kabla ya  kugonga jengo  lililo na afisi za gavana.

Lori hilo lililokuwa na                    nembo ya maduka ya jumla ya khetias lilikuwa limebeba bidhaa za duka.Aliyeshuhudia amesema dereva wa lori hilo hakuwa ndani wakati ajali hiyo ilipotokea akiongeza kuwa  huenda lori hilo lilibingiria  kutokana na uzito wa mizigo lililokuwa limebabe.

Hata haikubainika haraka iwapo dereva alikuwa ametumia breki.Askari wa kaunti ya lkakamega wamelaumiwa kwa kuyaruhusu magari kugezwa kwenye maeneo yasiyohitajika.

 

 

 

 

 

 

 

 

March 11, 2023