BY ISAYA BURUGU 29TH AUG 2023-Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameachiliwa huru katika kesi aliyoshtakiwa kuhusiana na kumpiga risasi Felix Orinda, maarufu kama Dj Evolve.

Haya yanajiri baada ya DJ Evolve kutoa ushahidi wake mahakamani na kuwasilisha kwamba hakuona mbunge huyo akiwa na bunduki wakati wa kisa cha risasi kilichotokea katika klabu ya usiku ya Nairobi mnamo Januari 2020.

Akitoa ushahidi wake akiwa kitandani, DJ huyo alisema hajui kilichompata kwani alijikuta tu kwenye gari la wagonjwa.

Hata hivyo alikiri katika mahakama ya Nairobi kwamba kweli alipigwa risasi na kujeruhiwa kwa risasi siku ya maafa, lakini hajui ni bunduki gani.Katika kesi hiyo, Babu Owino alikuwa ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya bunduki.

 

 

 

 

 

Share the love
August 29, 2023