Radio Osotua › Local News

Mataifa ya Afrika yatakiwa kuungana katika nyanja mbali mbali kwa manufaa ya kila mmoja

Local News June 24, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU 24TH JUNE 2023- Mataifa ya bara Afrika yametakiwa kuungana katika Nyanja mbali mbali kwa faiada ya kila mmoja.Wito huu umetolewa na mkewe naibu rais Rigathi Gachagua Bi Dorcas Gachagua.

Akizungumza katika taiafa Jirani la Uganda Dorcas amesisitiza umuhimu wa mataiafa ya Afrika kuondoa vikwazo na mipka ikiwemo kuendesha biashara kama njia oja ya kuhakikisha kuwa biashara na uchumi wa Afrika inainuka.

Mkewe naibu rais amesisitiza kuwa bara afrika lina uwezo wa kijisimamia na kujiendleza kutokana na rasilimali nyingi zilizoko kwenye bara hili.