Baraza la vyombo vya habari nchini limetaka vituo vya habari kutoa idhibati ya picha au kanda za video zinazoonyesha maafisa wa polisi waliozingira boma la Waziri wa zamani wa maswala ya ndani Dkt. Fred Matiang’i.

Katika barua yake MCK imeeleza kuwa taarifa za vyombo vya habari kuhusu kuzingirwa kwa boma la Waziri huyo wa zamani, Pamoja na taarifa kutoka kwa idara za usalama zilizopinga operesheni yoyote katika boma hilo, zinachanganya wakenya, jambo ambalo amesema huenda likachochea hali iya shauku na msukosuko wa kisiasa humu nchini.

Mkurugenzi mkuu wa MCK David Omwyoyo ameandika waraka kwa baadhi ya vituo vilivyochapisha taarifa hizo akieleza kuwa ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wakenya hawatapokezwa taarifa za uongo.

https://twitter.com/MediaCouncilK/status/1624392062484316160?s=20

February 11, 2023