Baraza la Vyombo vya Habari nchini (MCK) limeibua wasiwasi kuhusu kuendelea kushambuliwa kwa maneno kwa vyombo vya habari na maafisa wa serikali, likisema hulka hii inahujumu jukumu la vyombo vya habari kwa umma.

Katika taarifa ya baraza hilo iliyochapishwa hii leo, mkurugenzi mtendaji wa MCK David Omwoyo amewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kutoa cheche kali za maneno dhidi ya vyombo vya habari katika mikutano ya hadhara, akisema kauli za aina hii zinahatarisha Maisha ya wanachama wake na  pia linaondoa imani ya wananchi kwa vyombo vya habari katika jukumu lake kama mlinzi wa jamii.

February 24, 2023