BY ISAYA BURUGU 4TH SEPT 2023-Hali ya huzuni na majonzi imekumba Kijiji cha Kamahuru katika eneo bunge la tetu kaunti ya Nyeri baada ya msichana wa miaka 19 kuawa na mwili wake kutupwa katika shamba moja eneo hilo.

Msichana huyo anasemekana kupotea hiyo jana jumapili usiku kabla ya mwili wake kupatikana hivi leo asubuhi.

Wenyeji wanawataka polisi kuongeza upigaji wa doria nyakati za usiku sawa na kuwekwa mataa ya barabarani ili kuzuia visa kama hivyo siku zijazo.

Pia wamewataka maafisa wa polisi kufanya kila wawezalo ili kuwapata waliotekeleza mauji hayo.Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Nyeri

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 4, 2023