Mkuu wa mawaziri nchini Musalia Mudavadi, amewataka wahusika wote katika sekta ya Teknolojia na mawasiliano pamoja na vijana wenye ujuzi wa masuala ya teknolojia kunyakua fursa zinazopatikana katika anga ya kidijitali ili kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, na pia kuliweka taifa kwenye ramani ya ulimwengu kuhusu masuala ya kiteknolojia.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa awamu ya 12 ya kongamano la Connect Summit katika kaunti ya Kwale, Mudavadi alisisitiza haja ya ubunifu endelevu wa kiteknolojia ambao utaimarisha ukuaji wa uchumi wa Kenya, na pia kufungua nafasi sawa kwa wanaume na pia wanawake nchini.
Mudavadi vilevile alisisitiza haja ya kukumbatia suluhu za kidijitali zitakazosaidia kutatua matatizo nchini na pia kupunguza maswala ya ufisadi.
https://twitter.com/MusaliaMudavadi/status/1642902687451607041?s=20