Radio Osotua › Local News

Naibu rais awahimiza MCA mlima Kenya kuunga mkono vita dhidi ya Pombe haramu.

Local News April 21, 2023 John Waicua

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka wawakilishiwadi na viongozi wa maeneo ya mlima Kenya kuiunga mkono serikali katika vita vyake dhidi ya uraibu na ugemaji wa pombe haramu katika maeneo hayo.

Akizungumza katika kikao cha mashauriano na wawakilishiwadi kutoka katika kaunti za Nyeri, Kiambu, Murang’a, Kirinyaga na Nyandarua, Gachagua ameeleza kusikitishwa na idadi ya juu ya takwimu za vijana waliopotelea katika uraibu wa dawa hizi, huku akiahidi kuwa mipango ya kuondoa matatizo haya lazima ifanikiwe.