Radio Osotua › Local News

Naibu rais Gachagua awaonya wakuu wa utawala eneo la kati mwa nchi wanaoshirikiana na walanguzi wa dawa za kulevya

Local News April 14, 2023 Osotua

 BY ISAYA BURUGU 14TH APRIL,2023-NAIBU Rais Rigathi Gachagua hivi leo ameongoza mkutano wa wakuu wa utawala wakiwemo machifu, makamanda wa polisi nyanjani na kwenye kaunti eneo la kati mwa nchi ili kusaka suluhu kwa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya.

Mkutano huo umeandaliwa huko Nyeri kwa lengo la kutathmini mbinu mwafaka za kutatua tatizo hilo.

Akizungumza kwenye mkutano huo Gachagua amewataka wakuu hao wa utawala kuajibika  Zaidi  huku akisema kuwa wakati umefika kwa juhudi zote kuelekezwa katika kusaka suluhu.

Vilevile naibu rais ameonekana kuwalenga wakuu wa utawala wakiwemo machifu kufuatia kile alichokitaja kuwa ni wao kushirikiana  wagemaji pombe haramu  katika eneo hilo  hali ambayo imesambaratisha familia nyingi na kuharibu maisha.