Ofisi ya Kamishna wa Kulinda Data (ODPC) imefichua habari mpya kuhusu mradi tata wa sarafu ya Worldcoin, ikisema kuwa idadi ya Wakenya waliosajiliwa kwenye jukwaa hilo bado haijabainika.

Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya mawasiliano katika bunge la kitaifa, Kamishna wa Data Immaculate Kassait alieleza kuwa ofisi hiyo ya ulinzi wa data imeanza uchunguzi wa mashirika mengi ili kubaini hali halisi ya utendakazi wa Worldcoin.

Pia alisema kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini taarifa sahihi iliyokusanywa.

Aidha alisema kuwa Worldcoin ilipokea cheti cha usajili mnamo Aprili 2023 kwa sababu walitimiza mahitaji ya uendeshaji, ila hana ufahamu iwapo kampuni hiyo ilifanya kazi ndani ya mifumo ya kisheria iliyowekwa.

Share the love
August 15, 2023