BY ISAYA BURUGU 5TH SEP 2023-Polisi jijini Nairobi wamemkamata mshukiwa wa ujambazi aliyepia kiongozi wa genge la wahalifu linalosemekana kuwahangisha  wakazi wa Kayole katika Kaunti Ndogo ya Embakasi.

Kulingana na taarifa ya mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), mshukiwa, Luis Otieno almaarufu Lui Borura Nyaoiri, ambaye pia ana kesi inayosubiri kuwasilishwa mahakamani anaripotiwa kuhusika na visa vya wizi vilivyoripotiwa katika eneo hilo.

Lui alinaswa akiwa anaendesha gari la Mazda Demio linalodaiwa kuwa na nambari ghushi za usajili.

Baadaye aliwaongoza polisi  hadi nyumbani kwake ambapo bidhaa mbalimbali za thamani isiyojulikana zilipatikana zikiwa ni pamoja simu za mkononi,vipakatalishi,saa za mkononi  kati ya vitu vingine.

DCI anasema oparesheni ya kuwakamata washirika wake na kuwafikisha mahakamani inaendelea.

 

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 5, 2023