pembe za ndovu JKIA

Raia mmoja wa Indonesia amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) akiwa na pembe za ndovu zenye uzani wa kilo 38.4, zinazoaminika kuwa na thamani ya shilingi milioni 10. Mshukiwa huyo alinaswa na maafisa wa usalama kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KAA) kwa kushirikiana na Maafisa wa Kulinda Wanyamapori (KWS).

Pembe hizo ziligunduliwa baada ya uchunguzi wa kiusalama uliofanywa kwenye mizigo ya wasafiri katika Uwanja huo wa Ndege wa JKIA. Inaelezwa kwamba mshukiwa huyo alikuwa akielekea mjini Jakarta, nchini Indonesia, akitokea mji wa Bangui katika Taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

SOMA PIA: Wawili wakamatwa Embu na Pembe za Ndovu zenye Dhamani ya Milioni 10.

Uchunguzi unaendelea kuhusu jinsi mshukiwa huyo alivyozipata pamoja na lengo lake la kusafirisha nje ya taifa. Pembe za ndovu ni bidhaa zinazopigwa marufuku kimataifa na zina thamani kubwa kwenye soko la black market.

 

Share the love
October 10, 2023