Radio Osotua › Narok County

Rais Ruto Ampongeza Keter kwa Kushinda Uteuzi wa UDA Emurua Dikirr

Narok County March 28, 2026 Brigit Agwenge

Rais William Ruto amempongeza David Keter, anayejulikana pia kama Dollarline, kwa kushinda uteuzi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika eneobunge la Emurua Dikirr.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Rais alisema Keter ana uungwaji mkono kamili wa chama hicho anapojiandaa kushiriki uchaguzi mdogo ujao.

Rais pia alimtambua Bernard Ng’eno, maarufu kama Buluu, kwa kuendesha kampeni yenye ushindani mkubwa, akisema hatua hiyo imeimarisha demokrasia ndani ya chama.

Keter alijizolea ushindi huo baada ya mchuano mkali wa kura za maoni uliofanyika kuelekea uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Mei 14.

Kwa mujibu wa matokeo ya uteuzi huo, Keter alipata kura 13,749 na kufanikiwa kupata tiketi ya chama cha UDA, huku mpinzani wake wa karibu Bernard Kipkoech Ngeno akipata kura 13,394.