Radio Osotua › Local News

Rais Ruto arejea nchini baada ya ziara ya siku nne nchini Ujerumani na Ubelgiji

Local News March 30, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,30TH MARCH,2023-Rais  William Ruto amerejea nchini  baada ya ziara ya siku nnne nchini Ujerumaini na Ubelgiji.Rais aliondoka nchini Jumapili.Ndege iliyomeba rais na ujumbe wake imetua katika uwanja wa ndege wa jomo Kenyatta  jijini Nairobi ambapo amepokelewa  na naibu rais Rigatthi Gachagua.

Ziara ya Ruto aliguzia  kusisitiza kujitolea kwa Kenya katika  kuboresha mazungumzo yakimkakati na umoja wa ulaya Pamoja na uboreshwaji uhusiano  kati ya Kenya na umoja huo wa ulaya.

Akiwa nchini ujerumani rais alikutana na rais Frank-Walter Steinmeier  na chanzela wa ujerumani  Olaf Scholz kwenye mazungumzo  yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kibiasha kati ya Kenya na ujerumani.

Rais Ruto pia alihutubia kikao cha mjadala wa mageuzi ya kawi wa Berlin  huku akielezea changamoto za ukosefu wa kawi  wakati ulimwengu unashuhudia adhari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa na kushinikiza kuongezwa kwa uwekezaji katika kawi safi kwa Kenya na Afrika.