Rais William Ruto anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya kikazi kwa siku tatu katika kaunti za Kisii na Nyamira Pamoja na Maeneo bunge ya Kuria magharibi na Kuria Mashariki kuanzia hapo kesho.

Kulingana na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, ratiba ya Rais itaangazia uzinduzi wa miradi kadhaa katika eneo hilo kuambatana na ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza ya kuimarisha uchumi.

Akiwahutubia waandishi wa habari alasiri ya leo katika kaunti ya Kisii, msemaji wa Ikulu aliweka bayana kwamba rais atazindua ujenzi wa barabara ya kilomita 33 katika eneo hilo, Pamoja na kuanzisha miradi kadhaa ya maji katika kaunti ya Kisii.

https://twitter.com/HusseinMohamedg/status/1638528471491026945?s=20

March 22, 2023