BY ISAYA BURUGU 26TH OCT,2023-Sekta ya elimu nchini imepigwa jeki baada yar ais Wiliam Ruto kuzindua magari yatakayotumiwa na maafisa wa elimu katika kaunti zote 47 nchini kufuatilia utenda kazi wa sekta ya elimu.

Rais akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa katika chuo cha elimu maalum nchini eneo la Kasarani Nairobi,amesema kuwa seriakli yake iko imara kuhakikisha kuwa kila mtoto anapokea elimu bora.

Ni kupitia moyo huo ambao serikali imewajiri walimu alfu 56 zaidi na pia kuboresha mazingira ya kusomea Watoto kote nchini.Rais pia amewataka maafisa wa elimu nchini kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa lengo la serikali katika elimu limeafikiwa.

Magari hayo pia yatasaidia kusambaza vifaa vya mtihani wa kitaiafa wiki ijayo na kuhakikisha usimamizi bora

.Rais pia amerejelea azimio la serikali yake kuhakikisha kuwa mpango wa chakula  shueni unatekelezwa.

 

Share the love
October 26, 2023