Ruto Kuria

BY ISAYA BURUGU, 9TH NOV,2023-Rais William Ruto leo alasiri atatoa hotuba yake ya kwanza kabisa kuhusu Hali ya Taifa tangu achukue mamlaka mnamo Septemba mwaka jana.

Rais atahutubia kikao cha pamoja cha Bunge  la Kitaifa na Seneti.Maspika kutoka mabunge yote mawili, Moses Wetang’ula (Bunge la Kitaifa) na Amason Kingi (Seneti) walikuwa wametoa wito kwa wanachama wote kujitokeza katika majengo ya Bunge. Hotuba hiyo itakuja miezi 14 baada ya Ruto kuwa Rais wa tano wa Kenya.

Hotuba ya mwisho ya Hali ya Kitaifa ilitolewa na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Novemba 30, 2021.Hii ilikuwa miezi kadhaa kabla ya Uchaguzi Mkuu, ambapo Ruto aliibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha urais na kuapishwa rasmi Septemba 13, 2022.

Ibara ya 132 ya Katiba inasema kuwa; Mara moja kwa mwaka, ripoti, katika hotuba kwa taifa, kuhusu hatua zote zilizochukuliwa na maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya  za kitaifa.

Hotuba hiyo inajiri wakati ambapo kuna vilio vya Wakenya kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha tangu utawala wa Kenya Kwanza kuchukua madaraka.

Serikali ilikuwa tayari imetuma ujumbe wazi kuhusu jinsi itakavyokabiliana na gharama ya maisha.

Share the love
November 9, 2023