Rais William Ruto amekanusha vikali madai kuhusu nia ya serikali kubinafsisha huduma za Bandari ya Mombasa.

Akizungumza katika kikao cha kitaifa cha wajumbe wa chama cha UDA kilichoandaliwa katika ukumbi wa Bomas Jijini Nairobi siku ya Ijumaa, Rais Ruto amesisitiza kuwa serikali yake haina mpango wa kubinafsisha Bandari ya Mombasa. Badala yake, ameelezea dhamira ya serikali yake kuimarisha huduma za bandari hiyo ili kuendelea kutoa huduma bora hata kwa mataifa mengine katika ukanda wa Afrika Mashariki yanayotegemea huduma za bandari hiyo.

Katika hotuba yake, Rais Ruto alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na sekta ya kibinafsi katika juhudi za kuendeleza Bandari ya Mombasa. Alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuboresha miundombinu ya bandari, ufanisi wa utendaji, na kuiwezesha kushughulikia mzigo mkubwa wa biashara unaozidi kuongezeka katika eneo hilo.


 

Share the love
September 29, 2023