Rais William Ruto hii leo ametoa hotuba yake ya kwanza kwa taifa miezi 14 baada ya kutwaa madaraka.

Miongoni mwa masuala ambayo amezungumzia ni pamoja na gharama ya maisha. Rais Ruto amesema kuwa serikali yake imejitolea kuhakikisha kuwa gharama ya maisha inarudi chini ili kuwaokoa wananchi wa mapato ya chini.

Kuhusiana na suala la mazungumzo ya kitaifa, rais Ruto ameipongeza kamati hiyo na kueleza kuwa mazungumzo hayo yamechangia viongozi  kupata muafaka ju ya mambo mengi ambayo azimio lake litaharakisha mabadiliko yetu.

Ruto vilevile amesema kuwa mfumo wa elimu lazima utengeneze hazina kubwa ya ustadi, talanta, na rasilimali watu yenye ushindani na ubunifu ili kuunga mkono maono  ya Kenya iliyobadilika kiuchumi.

Share the love
November 9, 2023