Serikali imetenga Ksh. bilioni 1 itakayotumika katika zoezi la usajili wa vitambulisho vipya vya kidijitali kwa Wakenya wote.

Katibu Mkuu wa Uhamiaji Julius Bitok amesema kuwa vitambulisho hivyo ambavyo vitatolewa kwa raia wote vinanuiwa kuondoa vitambulisho vinavyotumika kwa sasa.

Akizungumza baada ya kukutana na Kamati ya Kitaifa ya Kitaalam ya Kitambulisho cha Kidijitali, Bitok alisema Wakenya watakaofikisha umri wa miaka 18 watapewa kitambulisho hicho iliyopewa jina la Maisha namba.

Zoezi hilo litazinduliwa rasmi tarehe 29 mwezi huu.

Share the love
September 12, 2023