Radio Osotua › Local News

Serikali yasema haitalegeza kamba katika vita dhidi ya wahalifu kaskazini mwa bonde la ufa.

Local News March 10, 2023 Brigit Agwenge

Rais William Ruto ameagiza maafisa wa kijeshi kushirikiana na wizara ya elimu ili kujenga upya shule zilizoharibiwa na wahalifu kaskazini mwa bonde la ufa.

Rais aliyasema haya kwenye hafla ya kufuzu kwa mahafala wa cadet wa kijeshi 330 katika shule ya kijeshi ya Lanet ilioko Nakuru.

ali kadhalika ametetea oparesheni ya kijeshi inayoendelea katika kaunti za Samburu, pokot magharibi, Laikipia, Elgeyo Marakwet na Turkana.