Radio Osotua › Local News

Shirika la Amnesty international lawataka wakaazi wa Kibra kuungana kujenga makanisa yaliyoharibiwa na wahuni,polisi wakilaumiwa kwa kutoajibika

Local News March 28, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,28TH MARCH,2023-Shirika la kutetea haki za kibinadamu umu nchini Amnesty International limekashfu uvamizi na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa katika mtaa wa kibra jijini Nairobi.Kupitia mkurugenzi wake mkuu Haningtone Irungu amewalaumu maafisa wa polisi kwa kutazama bila kufanya chochote wakati uvamizi na uaribifu huo ukitekelezwa

.Pia afisa huyo amewataka waumini wa kislamu kuwasaidia wenzao wakristu kujenga kanisa lililoharibiwa kwenye mtaa huo sawa  na kuwataka wakristu kuungana kusaidia ujenzi wa msikiti uliyoharibiwa katika ghasia za mandamano ya mungano wa Azimio.