Tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC imetangaza Agosti tarehe 10 mwaka wa 2027 kama tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Mpango wa Uendeshaji wa Uchaguzi (EOP) 2025–2027, Kamishna Ann Nderitu, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa Uchaguzi, alisema mfumo dhabiti umeundwa ili kuhakikisha uendeshaji mzuri wa uchaguzi.
Kamishna Nderitu aliongeza kuwa kampeni zimeratibiwa kuanza rasmi tarehe 29 mwezi Mei hadi Agosti 7 mwaka huo wa 2027.
Vyama vya kisiasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu lazima viwasilishe majina ya wagombea wanaotafuta tikiti ya chama kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi 16.
Nderitu alisema zaidi kwamba vyama lazima vikamilishe kura zao za mchujo na kutatua migogoro yote ya ndani ya vyama ifikapo Jumapili, Mei 9, 2027.
Wagombea ambao watashindwa kuwasilisha majina yao ndani ya ratiba zilizowekwa hawatasajiliwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.
Political Parties shall submit the Party Membership lists to the Commission on or before Tuesday, 16th March, 2027.
Political parties intending to present candidates in the General Election shall submit the names of persons contesting in the party primaries, the date and venues… pic.twitter.com/Rqx7KF3Pxc— IEBC (@IEBCKenya) June 24, 2026

