BY ISAYA BURUGU 26TH JULY 2023- Rais Wiliam Ruto yupo nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa kimataiafa wa rasilimali watu.Kwenye hotuba yake ya ufunguzi,rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasani amelezea umuhimuwa kuwekeza haswa kwenye vijana anaosema wana uwezo mkubwa wa kuinua mstakabali wa bara la Afrika.

Rais amesema bali na ukuaji wa kiuchumi ulioafikiwa katika mataiafa mbali mbali katika bara hili,kuna mengi yanayopaswa kufanywa ili kuleta maendeleo kwa viwango sawa.

Rais huyo hususan amesisitiza malengo manne yanayopasa kupewa kipau mbele.Kwa mjibu war ais Suluhu Ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya idadi ya watu barani afrika ni vijana,ni sharti hatua za makusudi kuchukuliwa katika kuwekeza kwenye miradi inayofaa kundi hili la watu la sivyo huenda hali ikageuka na kuwa balaa.

July 26, 2023