Baraza la Vyombo vya Habari nchini MCK limewataka wahariri kutekeleza wajibu wao kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari nchini ili kuimarisha taaluma katika tasnia ya habari.

Afisa mkuu mtendaji wa MCK Bw.David Omwoyo aliwataka wahariri kuhakikisha kuwa taarifa za wanahabari ni sahihi na zenye uwiano huku akiwahimiza wahariri kuwa kwenye msitari wa mbele katika utoaji wa taarifa sahihi, akisema nafasi ya vyombo vya habari imevamiwa na habari za uwongo na upotoshaji hatua ambayo imechangia watazamaji kutafuta uhakiki kutoka vyanzo vya kuaminika tofauti na waandishi wa habari.

Kando na hayo alithibitisha dhamira ya Baraza hilo kufanya vikao vingi vya wadau ili kushiriki na kuelewa madhara yanayosababishwa na kuripotiwa vibaya kwa habari.

Share the love
October 9, 2023