Wakenya wanatarajiwa kutumia zaidi kwenye chakula na bidhaa muhimu za matumizi ya nyumbani, ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupikia na unga wa ngano, kulingana na utafiti uliofanywa na CBK.
Haya ni kulingana na utafiti uliotolewa mnamo Juni 2026, ambao ulifanywa miongoni mwa wadau wa sekta ya kilimo, sukari, unga wa mahindi, na mchele, bidhaa zinazotarajiwa kuandikisha ongezeko la bei kuanzia Juni.
Wakulima walioshiriki katika utafiti wa Mei walihusisha ongezeko linalotarajiwa la bei na kupanda kwa gharama za usafirishaji kufuatia marekebisho ya hivi karibuni ya bei ya mafuta na EPRA.
Kwa sasa, lita tatu ya mafuta ya kupikia inauzwa kati ya Ksh800 na Ksh950, kulingana na chapa.
Pakiti ya kilo 2 ya unga wa ngano inauzwa kati ya Ksh158 na Ksh190, kulingana na chapa.
Wakati huo huo, pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi inagharimu kati ya Ksh150 na Ksh210 katika maduka makubwa mbalimbali, huku pakiti ya kilo 2 ya sukari ikiwa wastani wa takriban Ksh305.
Kwa upande mwingine, bei ya baadhi ya vyakula, hasa mboga, zinatarajiwa kushuka kutokana na ongezeko la usambazaji.
Miongoni mwa bidhaa zinazotarajiwa kuwa nafuu ni pamoja na sukuma, mchicha, na mboga za kienyeji.

