Radio Osotua › Local News

Wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi ya Ilmashariani mjini Narok wandamana kupinga kuhamishwa kwa mwalimu wao mkuu

Local News May 17, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU 17TH MAY 2023-Wanafunzi pamoja na  wazazi wa shule ya msingi ya Ilmashariani viungani mwa mji wa Narok wamefanya mandamano leo kupinga hatua ya kuhamishwa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Jane Sankok.

wakizungumza na wandishi wa habari wazazi pamoja na wanafunzi wamepinga hatua hiyo wakimtaja Bi Sankok kama mchapa kazi na bado hajatimiza miradi ya maendeleo katika shule hiyo

. Kwa mjibu wa Wazazi hao bi  Sankok yuko mbioni  kutekeleza miradi mingi yakimaendeleo aliyoanzisha n ani sharti apewe muda..