Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amepiga marufuku mikutano ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza chini ya mpango wake wa kuwafikia watu kwa jina Okolea.

Agizo hilo linakuja baada ya fujo kushuhudiwa Jumapili iliyopita wakati wa hafla ya Mwangaza ya ‘Mpango wa Okolea’ huko Makiri eneobunge la Igembe Kusini.

Akizungumza katika eneo bunge la Igembe ya Kati, Kindiki alitaja mikutano ya Okolea kuwa ya uchochezi.Aliwashutumu wafuasi wa Mwangaza kwa kuanzisha fujo, na kusababisha kulipiza kisasi kutoka kwa wapinzani.

Share the love
September 23, 2023