Chanjo

    Wizara ya Afya imetangaza kukamilika kwa mafanikio kwa kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya homa ya matumbo (Typhoid) na Surua-Rubella, iliyomalizika rasmi jana, ikiwa moja ya kampeni kubwa zaidi za chanjo katika historia ya Kenya.

    Katika kampeni hiyo ya siku 10, watoto zaidi ya milioni 16.1 walipokea chanjo ya Typhoid, na kufikia uchanjaji wa kitaifa wa asilimia 84, huku zaidi ya watoto milioni 5.18 wakipokea chanjo dhidi ya Surua na Rubella, na kufikia uchanjaji wa asilimia 81 dhidi ya kiwango cha kitaifa.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, kampeni hii ilishuhudia mwitikio chanya kutoka kwa wananchi kote nchini, ikiwa hatua muhimu katika kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki bila kinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo. Aidha, zaidi ya watoto 74,000 ambao hawajawahi kupokea chanjo yoyote ya kawaida hapo awali waliweza kubainika na kuchanjwa katika zoezi hili, ikiwa ni hatua muhimu katika juhudi za serikali za kuhakikisha kila mtoto analindwa.

    Wizara imethibitisha kuwa chanjo ya Typhoid sasa itapatikana bila malipo katika vituo vyote vya afya vya kutoa chanjo nchini, ili kuhakikisha ulinzi endelevu wa watoto wote

    July 16, 2025

    Leave a Comment