Katibu wa Kitaifa wa Chama tawala cha UDA, Cleophas Malala, amekanusha uvumi wa kuwepo nyufa ndani ya chama hicho. Akizungumza wakati wa ziara yake ya ufunguzi wa ofisi za chama mjini Narok siku ya Ijumaa, Malala amesisitIza kuwa hakuna chochote kinachowababaisha katika…
Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametoa amri ya kuwaua wahalifu wowote wanaolenga maafisa wa usalama au kambi za usalama. Akizungumza alipokuwa akizindua kambi ya GSU katika Eneo Bunge la Tiaty, Kaunti ya Baringo, Kindiki alisema mhalifu yeyote atakaye mpiga risasi…
Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa imeongeza muda wa agizo la kukizuia chama cha ODM kuwatimua Seneta wa Kisumu Tom Ojienda na wabunge Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o na Elisha Odhiambo kutoka kwa chama hicho. Mahakama hiyo pia iliagiza kesi hiyo itajwe…
Maafisa wa polisi katika kituo cha Olposimoru, Narok Kaskazini, wamemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumwua mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 12 katika kijiji cha Kipendeni eneo la Olengape. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa Idara ya Upelelezi…
Jeremiah Kioni bado anaaminika kuwa Katibu Mkuu halali wa chama cha Jubilee kulingana na utafiti uliofanya na TIFA. Katika utafiti huo uliotolewa leo Alhamisi, asilimia 32% ya waliohojiwa wanamtambua Kioni kama katibu mkuu wa Jubilee huku 21% wakimchukulia Kega kama katibu mkuu…
Serikali ya Kaunti ya Narok kupitia afisi ya kilimo na mifugo imeonya wafugaji eneo la Narok Magharibi hasa Endonyorasha kusitisha usafirishaji mifugo ili kutoa nafasi kwa maafisa wa afya kutoa chanjo dhidi ya mkurupuko wa ugonjwa wa kimeta yaani Anthrax. Akiongea na…
Maafisa wa polisi katika eneo la Kilifi wamewatia nguvuni mwanaume na mke wake, wanaodaiwa kuhusika na vifo vya watoto wao wawili kwa kukataa kuwapeleka hospitalini ili kupokea huduma za matibabu. Tukio hili la kusikitisha limejitokeza baada ya wazazi hao kukataa kuwapeleka hospitalini…
Serikali ya Kenya imechukua hatua za dharura kwa kushirikiana na idara mbalimbali na serikali za kaunti, ili kuhakikisha kuwa maandalizi ya mitihani ya kitaifa yanafanyika kwa ufanisi mwishoni mwa muhula huu. Hatua hii inakuja wakati ambapo maeneo mengi ya taifa yanatarajiwa kukumbwa…