Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imechapisha rasmi majina ya washindi wa uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliyopita, hatua inayowapa nafasi viongozi hao kuapishwa na kuanza rasmi majukumu yao. Majina hayo yalichapishwa katika toleo la jana la Gazeti Rasmi la Serikali.
Tayari bunge la kitaifa limedhibitisha kuwa wabunge waliochaguliwa wataapishwa hii leo kuanza shughuli za kuwahudumia wananchi.
Kwa mujibu wa IEBC, jumla ya viongozi 22 wamethibitishwa kuwa washindi, wakiwemo mmoja wa Seneti, sita wa Bunge la Kitaifa na 15 wa Bunge la Kaunti.
Katika nafasi ya Seneti, Kiprono Chemitei ametangazwa kuwa Seneta mteule wa Kaunti ya Baringo, akiwakilisha chama cha United Democratic Alliance (UDA).
Kwa upande wa Bunge la Kitaifa, waliothibitishwa ni:
Harrison Kombe (Magarini) – Orange Democratic Movement (ODM)
Ahmed Maalim (Banissa) – UDA
Leo Wa Muthende (Mbeere Kaskazini) – UDA
David Ndakwa (Malava) – UDA
Moses Omondi (Ugunja) – ODM
Boyd Were (Kasipul) – ODM
Katika Bunge la Kaunti, miongoni mwa wawakilishi wadi 15 waliotangazwa ni Douglas Masikonde wa Narok Mjini, akiwania kwa tiketi ya chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP). Orodha kamili ya wawaikilishiwadi inajumuishaUchaguzi Masikonde
Sophia Hamadawa (Chewani, Tana River) – UDA
Hassan Aden (Fafi, Garissa) – UDA
Antony Kyalo (Mumbuni North, Machakos) – Wiper Patriotic Front (WPF)
John Namesek (Lakezone, Turkana) – UDA
Cosmas Longor (Nanaam, Turkana) – UDA
Isabella Leshimirop (Angata Nanyokie, Samburu) – UDA
Vincent Kiplimo (Chemundu/Kapng’etuny, Nandi) – UDA
Douglas Masikonde (Narok Town, Narok) – Democracy for the Citizens Party (DCP)
Amos Maayial (Purko, Kajiado) – UDA
Dickson Aduda (Kisa East, Kakamega) – Democracy for the Citizens Party (DCP)
Eric Wekesa (Kabuchai/Chwele, Bungoma) – Independent
Christopher Moturi (Nyamaiya, Nyamira) – United Progressive Alliance (UPA)
Jeremiah Njenga (Ekeron’yo, Nyamira) – UPA
Jackson Mogusu (Nyansiongo, Nyamira) – Peoples Democratic Party (PDP)
David Wanyoike (Kariobangi North, Nairobi) – Democracy for the Citizens Party (DCP)
Hata hivyo, tangazo hilo la IEBC limejiri huku vyama vya upinzani vikiahidi kuelekea mahakamani kupinga matokeo ya maeneo ya Mbeere Kaskazini na Malava, ambako vinadai kuwepo kwa ukiukaji wa taratibu za uchaguzi.

