Radio Osotua › Local News

Ann Njeri akosa kufika bungeni huku uchunguzi wa shehena ya mafuta ya shilingi bilioni 17 ukiendelea

Local News November 22, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU 22ND NOV,2023-Ann Njeri Njoroge mwanamke aliye kwenye mzozo wa uagizaji wa mafuta ya shilingi bilioni 17 amekosa kufika mbele ya kamati ya kawi ya bunge la kitaifa huku wakili wake akisema kuwa ni mgonjwa na hawezi tembea.

Kamati ya kawi ya bunge la kitaifa inayochunguza Sakata ya umiliki wa mafuta hayo,imemwalika kwa mara ya pili Njeri kufika mbele yake huku ikijaribu kutanzua kitendawili kinachozunguka  Sakata hiyo.

Kamati hiyo imepa kufichua kiini cha mzozo juu ya mafuta hayo kati ya Njeri na wizara ya kawi.