Bei ya mafuta nchini haitabadilika kw akuongezeka au kupungua katika kipindi cha mwezi mmoja ujao. Taarifa kutoka kwa mamlaka ya udhibiti wa Nishati nchini imesema kuwa mafuta ya Super Petrol yataendelea kuuzwa kwa shilingi 177 kwa lita, Dizeli ikiuzwa kwa shilingi 162 kwa lita, na Mafuta ya Taa kwa shilingi 145.9 kwa lita, bei sawa na ile ambayo mafuta haya yalikua yakiuzwa mwezi Desemba mwaka jana.

January 14, 2023