Kiongozi wa upinzani kutoka taifa Jirani la Uganda Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine amesifia ujirani mwema wa taifa la Kenya na mataifa mengine ya jumuia ya Afrika Mashariki, hasa katika shughuli zao za kutetea haki na kupigania demokrasia katika mataifa wanachama.

Kyangulanyi alikua akizungumza katika kikao cha Pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika katika kaunti ya Mombasa. Kauli zake aidha zimeendelea kumchimba rasi wa Uganda Yoweri Museveni, akidokeza kuwa anaendelea kukandamiza demokrasia kila kuchao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi mkuu wa Haki Afrika Hussein Khalid amesisitiza haja ya kuungana ili kuendelea kutetea na kudumisha Demokrasia kwa mataifa yote, pamoja na kuhimiza demokrasia na uhuru katika taifa la Uganda. Khalid amesema kuwa ukuaji wa taifa la Uganda utawezesha pia taifa kukua hata Zaidi.

November 19, 2022