Jirongo

    Aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Vijijini na Mbunge wa Lugari, Cyrus Jirongo, ameaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani.

    Kwa mujibu wa taarifa, Jirongo alifariki papo hapo baada ya gari lake kugongana na basi la abiria lenye uwezo wa kubeba watu 45 katika barabara kuu ya Nairobi–Nakuru.

    Ajali hiyo ilitokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi, alipokuwa akirejea nyumbani kwake Lugari.

    Cyrus Jirongo, aliyekuwa na umri wa miaka 64, aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Maendeleo ya Vijijini wakati wa utawala wa Rais wa pili wa Kenya, Daniel arap Moi, kuanzia Machi 2002 hadi Desemba mwaka huo.

    Kisiasa, Jirongo alichaguliwa kuwa Mbunge wa Lugari kwa muhula wa kwanza kati ya mwaka 1997 na 2002, kisha kuhudumu kwa muhula wa pili kuanzia 2007 hadi 2013.

    Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, Jirongo aligombea kiti cha Ugavana wa Kaunti ya Kakamega kupitia chama cha United Democratic Party (UDP), lakini hakufanikiwa baada ya kushindwa na mgombea wa Orange Democratic Movement (ODM), Fernandes Barasa.

    December 13, 2025

    Leave a Comment