Kawira Mwangaza - seneti

BY ISAYA BURUGU,8TH NOV,2023-Gavana wa Meru anayekumbwa na utata  Kawira Mwangaza amebubujikwa na  machozi wakati wa kusikizwa kwa kesi yake ya kuondolewa mashtaka mbele ya Seneti.

Gavana alizua hisia kali huku akihojiwa na Wakili wake Elias Mutuma kuhusu baadhi ya matamshi yaliyotolewa dhidi yake hapo awali na viongozi wanaodaiwa kuhusika na jitihada za kumwondoa afisini.Ili kudhihirisha kwa njia dhahiri kwamba mashtaka hayo ni uwindaji wa  kisiasa, wakili wa gavana alitoa klipu kadhaa za video mbele ya kikao cha Seneti.Katika mojawapo ya video zilizomwacha Gavana na machozi, Mbunge wa Tigania Mashariki Mpuru Aburi anaswa akimshambulia kwa maneno kwa kutozaa na mumewe wa sasa.

.Alipoulizwa na wakili wake kuliambia Bunge la Seneti, kile ambacho mbunge huyo alikuwa akisema, Gavana Kawira anasema

:Wakili huyo anaendelea na kucheza klipu nyingine ambapo Naibu Gavana wa Kaunti ya Meru Isaac Mutuma ananaswa akifutilia mbali mpango tata wa Gavana unaoitwa Okolea ambapo amekuwa akitoa ng’ombe na magodoro kwa wakazi.

Katika klipu hiyo, naibu gavana, katika hafla ya hadhara, anaelezea kipindi cha Okolea kama programu ya umaskini inayowataka wenyeji wa Igembe Kusini ambako anatoka kukataa mpango huo.Katika kipande kingine Mbunge Mpuru Aburi anazidi kunaswa akihoji kabila la Gavana huyo, akiwataka wenyeji kumchagua kiongozi ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Meru.

Alipotakiwa kuelezea matamshi ya mbunge huyo, anasema: “Anasema baba wa Kawira Mwangaza anaitwa Njuguna na mama Mugure na hawataki kutawaliwa na Mkikuyu kule Meru na ndiyo maana wanataka kubadilika na kuwa Peter. Munya Gavana wa kwanza.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
November 8, 2023