BY ISAYA BURUGU,30TH NOV,2023 Rais Wiliam Ruto amesema Serikali  itawazawadi  Wakopaji wa Hustler Fund kwa 50% ya Akiba Yao.Vilevile Wakenya ambao wameweka akiba na Hazina ya Ushirikishwaji wa Kifedha, pia inajulikana kama Hustler Fund, watapata nyongeza ya asilimia 50 ya akiba yao ya muda mrefu.

Rais akizungumza katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanznishwa kwa hazina ya husler jijini Nairobi,rais amesema Chini ya mfuko huo, asilimia 5 ya kila mkopo inaelekezwa kwenye akiba; Asilimia 70 kwa akiba ya muda mrefu na asilimia 30 kwa akiba ya muda mfupi

.Ruto amesema hazina hiyo kufikia kesho  Ijumaa itawatuza wakopaji milioni 1.2 kwa kiwango kinacholingana  katika akaunti yao ya akiba ya muda mrefu katika uwiano wa shilingi 1 kwa kila shilingi mbili zinazookolewa.

Kulingana na rais, Hustler Fund kwa sasa inahudumia wateja milioni 21.8 waliojijumuisha, milioni 7.7 kati yao wamekuwa wateja wa kurudia.Alisema Wakenya wameokoa jumla ya Ksh.2 bilioni kutoka kwa mikopo yao kufikia sasa.Wakati uo huo, Rais Ruto alisema serikali sasa itaweka akiba ya muda mfupi kwa wateja ili kutoa urahisi zaidi na manufaa ya haraka kutokana na juhudi zao za kuweka akiba.

Ilizinduliwa mnamo Novemba 30, 2022, Hustler Fund inalenga Wakenya ambao hawakuweza kupata mikopo baada ya kuorodheshwa na mashirika mbalimbali ya kukadiria mikopo.Inatoa mikopo kutoka kima cha chini kabisa cha Ksh.500 hadi Ksh.50,000 kwa msingi wa asilimia nane au kiwango cha kila siku cha asilimia 0.002.

 

November 30, 2023