Hoja ya kumtimua Gavana wa Kaunti ya Isiolo, Abdi Guyo, itasikilizwa na vikao vya pamoja vya Bunge la Seneti, baada ya pendekezo la kuunda kamati maalum ya kushughulikia kesi hiyo kukataliwa katika vikao vya jana.
Spika wa Seneti, Amason Kingi, alitangaza kwamba vikao vya kusikiliza hoja hiyo vitaandaliwa tarehe 8 na 9 Julai mwaka huu.
Wiki iliyopita, Gavana Guyo alitimuliwa rasmi ofisini baada ya wawakilishi wadi 16 kati ya 18 kuunga mkono hoja ya kumbandua, iliyomhusisha na madai kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya afisi, uvunjaji wa Katiba, na kukwamisha miradi ya maendeleo katika Kaunti ya Isiolo.
Seneti inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu hatima yake baada ya kusikiliza pande zote mbili katika kikao hicho.