BY ISAYA BURUGU,9TH FEB,2023-Ibada ya Misa ya wafu kwa aliyekuwa Waziri wa elimu marehemu George Magoha imeandaliwa leo katika kanisa la Consolata shrine mtaani Westalands jijini Nairobi

.Ibaada hiyo iliyongozwa na askofu mkuu wa jimbo kuu la Nairobi Philip Anyolo imehudhuriwa na waliokuwa maafisa wakuu katika serikali iliyopita na wakiwemo mawaziri waliofanya kazi na Magoha sawa na maafisa wa serikali ya sasa.Wote waliozungumza kwenye hafla hiyo wamekumbuka mchango wa Magoha katika nyakai tofauti wakati akihudumu serikalini na hata katika Maisha yake yakibinafsi .

Kwenye ulogia yake Magoha amelezwa kuwa mtu aliyekuwa na mwelekeeo na aliyejitolea kufanikiwa katika kila kitu alichoguza au kutamania, bali na kumcha mwenyezi Mungu .

Magoha aliaga dunia Januari 24 katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri 71.Tangu kutangazwa kwa kifo chake viongozi mbalimbali wameitembelea familia yake kuipa rambirambi zao na kuomboleza nao. atazikwa katika eneo la Umiru‚ kaunti ndogo  ya Nyamininia jumamosi wiki hii.

 

 

 

 

 

 

February 9, 2023