Uchaguzi Masikonde

    Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imechapisha rasmi majina ya washindi wa uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliyopita, hatua inayowapa nafasi viongozi hao kuapishwa na kuanza rasmi majukumu yao. Majina hayo yalichapishwa katika toleo la jana la Gazeti Rasmi la Serikali.

    Tayari bunge la kitaifa limedhibitisha kuwa wabunge waliochaguliwa wataapishwa hii leo kuanza shughuli za kuwahudumia wananchi.

    Kwa mujibu wa IEBC, jumla ya viongozi 22 wamethibitishwa kuwa washindi, wakiwemo mmoja wa Seneti, sita wa Bunge la Kitaifa na 15 wa Bunge la Kaunti.

    Katika nafasi ya Seneti, Kiprono Chemitei ametangazwa kuwa Seneta mteule wa Kaunti ya Baringo, akiwakilisha chama cha United Democratic Alliance (UDA).

    Kwa upande wa Bunge la Kitaifa, waliothibitishwa ni:

    • Harrison Kombe (Magarini) – Orange Democratic Movement (ODM)

    • Ahmed Maalim (Banissa) – UDA

    • Leo Wa Muthende (Mbeere Kaskazini) – UDA

    • David Ndakwa (Malava) – UDA

    • Moses Omondi (Ugunja) – ODM

    • Boyd Were (Kasipul) – ODM

    Katika Bunge la Kaunti, miongoni mwa wawakilishi wadi 15 waliotangazwa ni Douglas Masikonde wa Narok Mjini, akiwania kwa tiketi ya chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP). Orodha kamili ya wawaikilishiwadi inajumuishaUchaguzi Masikonde

    • Sophia Hamadawa (Chewani, Tana River) – UDA

    • Hassan Aden (Fafi, Garissa) – UDA

    • Antony Kyalo (Mumbuni North, Machakos) – Wiper Patriotic Front (WPF)

    • John Namesek (Lakezone, Turkana) – UDA

    • Cosmas Longor (Nanaam, Turkana) – UDA

    • Isabella Leshimirop (Angata Nanyokie, Samburu) – UDA

    • Vincent Kiplimo (Chemundu/Kapng’etuny, Nandi) – UDA

    • Douglas Masikonde (Narok Town, Narok) – Democracy for the Citizens Party (DCP)

    • Amos Maayial (Purko, Kajiado) – UDA

    • Dickson Aduda (Kisa East, Kakamega) – Democracy for the Citizens Party (DCP)

    • Eric Wekesa (Kabuchai/Chwele, Bungoma) – Independent

    • Christopher Moturi (Nyamaiya, Nyamira) – United Progressive Alliance (UPA)

    • Jeremiah Njenga (Ekeron’yo, Nyamira) – UPA

    • Jackson Mogusu (Nyansiongo, Nyamira) – Peoples Democratic Party (PDP)

    • David Wanyoike (Kariobangi North, Nairobi) – Democracy for the Citizens Party (DCP)

    Hata hivyo, tangazo hilo la IEBC limejiri huku vyama vya upinzani vikiahidi kuelekea mahakamani kupinga matokeo ya maeneo ya Mbeere Kaskazini na Malava, ambako vinadai kuwepo kwa ukiukaji wa taratibu za uchaguzi.

    December 2, 2025

    Leave a Comment