Mafuriko

Watu 15 wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa humu nchini hadi kufikia sasa. Shirika la Msalaba Mwekundu nchini limetoa taarifa rasmi asubuhi ya leo, inayoeleza kuwa zaidi ya watu 15,264 wameathiriwa moja kwa moja na mvua kubwa inayoendelea, huku zaidi ya mifugo 1067 ikipoteza maisha katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Redcross, mafuriko haya yanasemekana kuwa yametokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya taifa. Zaidi ya ekari 241 zilizokuwa na mazao na vyakula zimeharibiwa na mafuriko, jambo linalosababisha wasiwasi wa upatikanaji wa chakula katika maeneo hayo.

Shirika hilo limeanzisha juhudi za kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko, ikiwa ni pamoja na huduma za dharura na misaada ya kibinadamu. Majuma kadhaa yaliyopita, idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini, ilitangaza kuwa maeneo mengi ya taifa yatashuhudia kiwano cha juu cha mvua. Kwa sasa idara hiyo inaonya kwamba mvua hii itaendelea hadi mwezi Januari mwakani.

SOMA PIA: Mvua Kubwa za El Nino Kushuhudiwa Kati ya Septemba na Oktoba.
Share the love
November 6, 2023